1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Zealand na Ujerumani zasaini mkataba mpya wa ushirikiano

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Ujerumani na New Zealand zimetia saini mkataba wa maelewano ya kukuza ushirikiano baina yao.

https://p.dw.com/p/4fVlX
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na Winston Peters mwenzie wa New Zealand
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na Winston Peters mwenzie wa New ZealandPicha: Sina Schuldt/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Winston Peters, amesema mkataba huo utaongeza uhusiano kati ya Ujerumani na New Zealand.

Mawaziri hao wawili pia walijadili haja ya kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza na kuimarisha ushirikiano katika eneo la Pasifiki. Peters alisema New Zealand na Ujerumani zinaamini kwenye maslahi na maadili ya pamoja, ikiwa ni pamoja na utawala wa sheria, demokrasia, heshima kwa mfumo wa kimataifa na haki za binaadamu.

Annalena Baerbock aliwasili New Zealand jana Ijumaa kutoka Australia. Hapo kesho Jumapili, Baerbock atatembelea kisiwa cha Fiji katika Pasifiki ya Kusini.