1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Makombora ya Urusi yaua watu wawili nchini Ukraine

5 Mei 2024

Shambulizi la roketi la Urusi katika eneo la mashariki mwa Ukraine la Donetsk limeua watu wawili huku shambulio la droni katika mji wa kaskazini mashariki wa Kharkiv likiwajeruhi wengine sita.

https://p.dw.com/p/4fWC7
Ukraine | Mashambulizi ya Urusi huko Donetsk
Maafisa wa afya wa Ukraine wakibeba mwili wa mwanajeshi baada ya shambulio la Urusi huko Donetsk: 16.03.2016Picha: Madeleine/ZUMA/IMAGO

Mashambulizi hayo ya jana usiku yalifanyika wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kwa Wakristo wa madhehebu ya Orthodox wa nchini  Ukraine na Urusi.

Hayo yakiarifwa, Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi ilirusha droni 24 zilizotengenezwa na Iran aina ya "Shahed" na kusisitiza kuwa 23 kati ya hizo zilidunguliwa.